Tommi na Terry
London,England.
Ukiachana na utemi wake uwanjani hasa katika kuwashughulikia washambuliaji wasumbufu John Terry ni mtu tofauti kabisa linapokuja suala la kusaidiwa watu wenye shida mbalimbali.
SIKIA HII
Nahodha wa Chelsea Muingereza John Terry amejitolea kugharamia gharama zote za mazishi ya shabiki wa Chelsea,Tommi Miller aliyefariki kwa ugonjwa wa Leukaemia.
Taarifa zinasema Terry amekubali kulipia kiasi chote cha £1,600 ambacho kinatakiwa kwa ajili ya kugharamia mazishi hayo baada ya kuombwa kufanya hivyo na rafiki wa familia ya Tommi aitwaye Tawney-Bianca Toogood.
Bianca Toogood alimtumia Terry ujumbe mfupi kupitia ukurasa wake wa Instagram na kumuomba asaidie kulipia gharama za mazishi ya shabiki yake kipenzi Tommi.
Tommi alifariki Machi 31 mwaka huu nyumbani kwao Thorpe Way,Cambridge baada ya madaktari kushindwa kupata tiba ya ugonjwa wake.
Mazishi ya Tommi yatafanyika siku ya alhamis huko Saint Mary the Virgin Parish Church.Watu watakaohudhuria mazishi hayo watatakiwa kuvaa jezi za Chelsea ama za Cambridge United vilabu ambavyo Tommi alikuwa akivishabikia enzi za uhai wake.
Tommi na Terry walikutana Juni mwaka jana baada ya Tommi kupata mwaliko wa kutembelea uwanja wa nyumbani wa Chelsea,Stamford Blidge.
Kwa mujibu wa mama wa marehemu,Tommi alikuwa akimhusudu sana John Terry pamoja na Peter Cech.
Tommi akiwa na wachezaji wa Chelsea
0 comments:
Post a Comment