Accra,Ghana.
Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) limemfungia maisha kutokujihusisha na shughulo za mpira wa miguu mwamuzi Joseph Lamptey raia wa Ghana.
Uamuzi huo umetolewa kufuatia Lamptey kutoa maamuzi ya utata ya penati kwa wenyeji Afrika Kusini dhidi ya Senegal katika mchezo wa kuwania tiketi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 uliochezwa Novemba 2016 mchini Afrika Kusini.
Kuna uwezekano wa mchezo huo kurudiwa endapo FIFA itajirizisha na uchunguzi zaidi unaondelea kuhusiana na maamuzi ya mchezo huo.
Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa kufuzu Kombe la Dunia, Afrika Kusini waliibuka na uhsindi wa mabao 2 – 1 dhdi ya Senegal, ambapo bao la kwanza la wenyeji la mkwaju wa penati liligubikwa na utata .
0 comments:
Post a Comment