Dar Es Salaam,Tanzania.
Kocha wa Timu ya Taifa Tanzania , Taifa Stars Salum Mayanga Leo baada ya timu ya Taifa stars kuanza kambi ametaja manahodha wa timu hiyo .
Msemaji wa TFF Ndugu Alfred Lucas ameiambia soka extra kuwa Kocha ametaja manahodha wa timu ya Taifa na amependekeza jina la mchezaji Mbwana Ally Samatta anayechezea klabu ya Genk iliyopo nchini Belgium kuwa ndio nahodha mkuu wa timu ya Taifa Stars .
Pia Mwalimu Mayanga amewataja Himid Mao Mkami na Jonas Gerrard Mkude kuwa ni Manahodha wasaidizi wa timu ya Taifa Tanzania .
" Itakapo cheza timu yetu ya Taifa kwenye mashindano yanayoandaliwa na FIFA Samatta atakuwa nahodha ila Timu ikicheza mashindano ya ndani basi Himid na Mkude Watakuwa manahodha kulingana na aina ya mashindano".Alfred Lucas aliongeza kuwa timu imeanza maandalizi mazuri kuelekea mechi ya kirafiki .
0 comments:
Post a Comment