Abidjan,Ivory Coast.
IVORY COAST imetangaza kumuajiri Mbelgiji,Marc Wilmots kuwa kocha mkuu wa timu yake ya taifa.
Wilmots,48,anachukua nafasi ya Mfaransa,Michel
Dussuyer aliyejiuzulu mwezi Januari baada ya Ivory Coast kufanya vibaya kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon mapema mwaka huu.
Wilmots amedaiwa kuingia mkataba wa miaka miwili na Ivory Coast huku akipewa sharti la kuhakikisha miamba hiyo ya Afrika Magharibi inakata tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika nchini Urusi vinginevyo kibarua chake kitaota nyasi.
Kabla ya kutua Ivory Coast , Wilmots alikuwa akiinoa timu ya taifa ya Ubelgiji.Ikiwa chini Wilmots,Ubelgiji ilishinda michezo 32 ikitoka sare mara 8 na kufungwa mchezo mmoja pekee katika michezo 50.
0 comments:
Post a Comment