Lameck Francis
Zanzibar
Waziri wa habari utalii na utamaduni Mh Rashid Ali Juma rasmi amekabithi Uwanja wa Mao Tse Tung kwa wakandarasi wa Kichina kampuni ya Zhengtar Group Company Limited hivi karibuni kwa ajili ya kuujenga uwanja wa kisasa ambao utajengwa kwa mwaka mmoja na miezi miwili kisiwani Unguja
kupitia kwa katibu mkuu wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar amesema Uwanja huo utagharimu Shilingi Bilioni 11.5 kwa fedha za Tanzania ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China itatoa Shilingi Bilioni 11.5 huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 ambazo ukijumlisha inakua Bilioni 12.5 ambazo watalipwa Wakandarasi wa uwanja huo ambao ni Kampuni ya Zhengtar Group Company Limited kutoka china ambayo ina uzoefu mkubwa wa kujenga Viwanja wa Michezo sehemu tofauti tofauti
katika hatua nyingine msimamizi wa serikali katika ujenzi wa uwanja huo Ali Mbarouk Juma amesema Ujenzi huo utakuwa na Viwanja viwili vya mpira wa miguu na kingine cha michezo ya ndani kama vile Mpira wa Kikapu na mazoezi
uwanja huo unategemea kubeba watazamaji zaidi ya 1500 watakao kaaa jukwaa kuu na jukwaa jingine watazamaji 900 pia kutakua na taa ambazo zitafanya ichezwe michezo hata wakati wa usiku
hii hapa chini ni picha ya namna uwanja utakavyokuwa
0 comments:
Post a Comment