Dar Es Salaam,Tanzania.
Yanga SC imepigwa faini ya Tsh 500,000 (Laki Tano) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mechi yao dhidi ya Simba iliyopigwa uwanja wa Taifa Feb,25,2017.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania (Kamati ya Saa 72), katika kikao chake cha Machi 4, mwaka huu kupitia matukio mbalimbali ya Ligi
Kuu msimu wa 2016/2017 unaoendelea sasa.
Imeelezwa kuwa kitendo hicho walichofanya Yanga ni kinyume cha kanuni ya 14(14) ya ligi kuu inayosema kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi.
0 comments:
Post a Comment