London, England.
DIEGO Costa (Pichani) akishangilia pamoja na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Chelsea bao la pili katika ushindi wa mabao 2-1dhidi ya West Ham United kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa Jumatatu usiku huko dimbani London Stadium.
Eden Hazard alianza kuifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika ya 25 kabla ya Diego Costa kufunga bao la pili muda mfupi kabla ya mapumziko.Bao la West Ham United limefungwa na kiungo wa Argentina,Manuel Lanzini.
Ushindi huo umeipa Chelsea rekodi ya kushinda michezo 21 kati ya michezo yake 27 ya ligi kuu England na kufikisha pointi 66,pointi 10 mbele ya Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya pili.Manchester
City wanaweza kupunguza tofauti hiyo ya pointi ikiwa wataibuka na ushindi dhidi ya Stoke City Jumatano.
Msimamo wa ligi kuu England kwa ufupi:
1. Chelsea 66
2. Tottenham 56
3. Man City 55
4. Liverpool 52
5. Arsenal 50
6.Man Utd 49
7.Everton 44
8.West Brom 40
9.Stoke City 35
10.Southampton 33
0 comments:
Post a Comment