Msafara wa klabu ya soka ya Yanga mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara , utaondoka alhamisi nchini kuelekea nchini Zambia katika mechi ya marudiano na Zanaco FC kwa Ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways.
Msafara wa Yanga SC utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi 7 . Yanga inaelekea Zambia katika mechi ya marudiano klabu bingwa Afrika baada ya mechi ya awali jumamosi kutoka sare ya 1-1 na Zanaco FC uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Timu inaendelea vyema na mazoezi kuelekea mchezo huo wa marudiano utakaochezwa siku ya Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment