Msalaba Bernard.
Bosi wa klabu ya Chelsea, Muitaliano Antonio Conte amegoma kuupa uzito mjadala wowote unaowahusisha viungo Ngolo kante wa Chelsea pamoja nae Paul Pogba wa Manchester United. Conte amewahi kumnoa Pogba akiwa Juventus.
Conte amedai si sahihi kuwalinganisha nyota hao kwani wako tofauti. Kante ambaye anang’ara na Chelsea kwasasa alitua klabuni hapo kwa kitita cha £32 million akitokea Leicester City ilihali mfaransa mwenzake Paul Pogba amerejea klabuni Manchester United kwa dau lilloweka rekodi ya dunia £89 million.
Conte amenukuliwa akisema “hawafanani, kila mmoja ana upekee wake,. Conte pia amemmwagiza sifa Pogba akisema “Paul niliyebahatika kumfundisha kwa misimu kadhaa ni mchezaji wa kiwango cha juu, ni mchezaji wa aina yake hata anapokuwa anafundishwa” “Paul daima atajitahidi kuwa bora zaidi, ana mbimu bora, ana stamina, yaani tunamzungumzia mchezaji wa daraja la juu”.
Chelsea inajiandaa kuvaana na Manchester United hapo kesho kunako robo fainali ya FA, huku Manchester United ikitaraji kumkosa mshambuliaji wake mahiri Zlatan Ibrahimovic aliyefungiwa mechi tatu kwa mchezo usio wa kiungwana dhidi ya Tyrone Mings wa Bournemouth wikiend ilpita.
Conte pia alimaliza kwa kusema mipango yake ni kuikabili Manchester jkama timu nzima na si Pogba pekee.
0 comments:
Post a Comment