728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, March 13, 2017

    Ukata,kocha wa kigeni vyaiondoa Malawi AFCON,CHAN

    Lilongwe,Malawi.

    MALAWI imetangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya CHAN ya mwaka 2018 na ile ya AFCON ya mwaka 2019 kutokana na kukabiliwa na ukata mkali wa kifedha pamoja na kushindwa kuajiri kocha wa kigeni.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama cha soka cha nchi hiyo (FAM),Malawi imeamua kujitoa kwenye michuano hiyo baada ya serikali ya nchi hiyo kukataa kutoa ruhusa kwa chama hicho kuajiri kocha wa kigeni kwa madai ya kutokuwa na fedha.

    Awali FAM ilipendekeza kuajiri kocha wa kigeni na kuiomba serikali iisaidie kuchangia asilimia hamsini (50) ya gharama za mshahara lakini baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa serikali ya Malawi kupitia kwa waziri wake wa michezo imetangaza kuupiga chini mpango huo.

    Malawi imekuwa haina kocha mkuu tangu Mrundi Nsanzurwimo Ramadhan alipoondoka mwezi Septemba mwaka 2016. Japo Malawi itakabiliwa na faini kutoka shirikisho la vyama vya soka Afrika (CAF) kutokana na kujiondoa huko,katibu mkuu wa FAM,Alfred Gunda amesema ni bora kulipa faini kuliko kushiriki katika michuano ambayo nchi haina uwezo wa kuigharamia.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ukata,kocha wa kigeni vyaiondoa Malawi AFCON,CHAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top