Masaka,Uganda.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC,Emmanuel Okwi,jana Jumapili aliibuka shujaa baada ya kuifungia SC Villa mabao matatu (hat-trick) katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Onduparaka FC kwenye mchezo wa ligi kuu Uganda uliochezwa kwenye uwanja wa Masaka recreation Ground.
Mabao hayo matatu (hat-trick) yamemfanya Okwi aungane na Allan Okello wa KCCA FC na kuwa wachezaji pekee waliofunga idadi hiyo ya mabao kwenye mchezo mmoja msimu huu.Wote wamefunga mabao hayo dhidi ya Onduparaka FC.
Ushindi huo umeifanya SC Villa kuungana na KCCA FC kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uganda.SC Villa ina michezo mitatu zaidi ya KCCA FC.
Matokeo Mengine:Bright Stars FC imetoka sare ya bao 1-1 na The Saints.Express FC imeichapa Kirinya Jinja SS 1-0.
0 comments:
Post a Comment