728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, March 13, 2017

    Zambia mabingwa wapya AFCON ya vijana

    Lusaka,Zambia.

    TIMU ya taifa ya vijana ya Zambia ya vijana walio chini ya umri wa miaka 20,Young Chipolopolo wametwaa ubingwa wa Afrika wa michuano hiyo baada ya jana Jumapili kuwafunga vijana wenzao wa Senegal kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka.

    Mabao ya ushindi ya Zambia kwenye mchezo huo ulioshuhudiwa pia na Rais wa nchi hiyo,Edgar Lungu,yamefungwa na Patson Daka pamoja na Edward Chilufya.Hii ni mara ya kwanza kwa Young Chipolopo kutwaa ubingwa wowote mkubwa wa Afrika.

    Michuano hiyo ilianza Februari 26 na kujumuisha timu nane zilizokuwa katika makundi mawili ya A na B.

    Kabla ya kufika fainali Zambia iliyokuwa kundi A iliichapa Guinea 1-0.Ikaifunga Mali 6-0 kisha ikafunga kazi kwa kuifumua Misri 3-0.Katika nusu fainali Zambia iliifunga Afrika Kusini 1-0.

    Senegal waliokuwa kundi B walianza safari ya kuelekea fainali kwa kutoka sare ya 1-1 na Sudan.Wakaifunga Afrika Kusini 4-3 kisha wakafunga kazi kwa kuifunga Cameroon 2-0. Katika nusu fainali Senegal iliichapa Guinea 1-0.

    Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliochezwa mapema jana Guinea iliibuka kidedea baada ya kuifumua Afrika Kusini 1-0.

    Timu zilizofika fainali zitaiwakilisha Afrika kwenye michuano ya vijana itakayofanyika Korea Kusini Mei mwaka huu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Zambia mabingwa wapya AFCON ya vijana Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top