Harare,Zimbabwe.
TP Mazembe Englebert imetupwa nje ya michuano ya klabu bingwa Afrika na kujikuta ikiangukia kwenye michuano ya shirikisho baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bila kufungana na mabingwa wa Zimbabwe,Caps United katika mchezo mkali wa marudiano wa hatua ya mtoano uliochezwa katika uwanja wa taifa wa Zimbabwe uliopo jijini Harare.
Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa Jumapili iliyopita huko Lubumbashi,DR Congo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.Caps United walipata bao kupitia kwa Abbas Amidu wakati bao la wenyeji TP Mazembe lilifungwa na nahodha wake,Rainford Kalaba.
0 comments:
Post a Comment