Sittard,Uholanzi.
NAHODHA na kocha wa zamani wa Nigeria,Sunday Oliseh ameimwagia sifa kemkem Barcelona kufuatia usiku wa kuamkia leo Alhamis kuing'oa Psg na kutinga robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupindua matokeo kutoka kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza na kupata ushindi wa jumla wa mabao 6-5 baada ya kushinda mabao 6-1 katika mchezo wa pili uliochezwa jana nyumbani Nou Camp.
Oliseh,43,ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya daraja la pili ya Fortuna Sittard ya Uholanzi ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ushindi wa Barcelona dhidi ya Psg ni maajabu katika mchezo wa soka.
“Ushindi huu wa Barcelona wa mabao 6-1,ni maajabu; ni mechi ambayo nitawasimulia wajukuu zangu kama Mungu ataruhusu".“Sidhani kama kutakuja kutokea tena mechi kama hii,Sidhani" Ameandika Oliseh aliyewahi kuvichezea vilabu vya Ajax, Juventus na Borussia Dortmund.
Jana Barcelona iliandika historia kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupindua kichapo cha mabao 4-0 ilichokipata wiki mbili zilizopita nchini Ufaransa na kushinda mabao 6-1 nyumbani Nou Camp.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez, Lionel Messi, Neymar aliyefunga mabao mawili.Sergi Roberto na bao la kujifunga la beki Layvin Kurzawa.Bao pekee la Psg limefungwa na Edison Cavani.
0 comments:
Post a Comment