Munich,Ujerumani.
Vilabu vya Arsenal na Bayern Munich zimeshitakiwa
na shirikisho la soka Ulaya (UEFA) kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu
vilivyoonyeshwa na mashabiki wao kwenye mchezo wao wa juzi Jumanne wa hatua ya
16 bora ya michuano ya michuano ya klabu bingwa Ulaya uliochezwa kwenye uwanja
wa Emirates jiijni London.
Bayern Munich imeingia hatiani baada ya
mashabiki wake kutupa vitu mbalimbali uwanjani ikiwemo vipande vya karatasi
hali iliyofanya mchezo uchelewe kwa dakika kadhaa.Mashabiki hao walikuwa
wakipinga tozo kubwa la viingilio kwenye mchezo huo.Pia mashabiki hao
walionekana wakiwa na bango lililosomeka "Bila ya mashabiki mchezo wa soka
ni bure kabisa"
Arsenal wao wameingia hatiani baada ya mmoja wa
mashabiki wao kuvamia uwanjani katika sehemu ya kuchezea katika mchezo huo
ulioisha kwa wenyeji Arsenal kulala kwa mabao 5-1.
UEFA pia imeitia hatiani Napoli kwa makosa
manne baada ya mashabiki wake kufanya fujo katika mchezo wake wa jana Jumanne
ambao miamba hiyo ya Italia ilichapwa mabao 3-1 na Real Madrid huko Stadio San
Paolo na kutupwa nje kwa jumla ya mabao 6-2.Katika mchezo wa awali uliochezwa
Hispania,Napoli ililala kwa mabao 3-1.
Baadhi ya makosa ambayo yameitia hatiani
Napoli ni pamoja na kutupa vitu mbalimbali uwanjani,uwashaji wa baruti,matumizi
ya laser pointer na kuziba ngazi za uwanjani.Mashtaka yote yatasikilizwa Machi
23 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment