Como,Italia.
MKE wa kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ghana,Michael Essien,bi Akosua Puni ameinunua timu ya Como FC inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Italia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Italia,Puni ameinunua timu hiyo kwa dau la Euro 237,000 (US$ 254,000) katika mnada uliofanyika hivi karibuni huko Como.
Bei hiyo haijumuishi uwanja wa mazoezi unaotumiwa na timu hiyo wala nembo ya timu hiyo Calcio Como.Wakati huohuo habari zinasema Como FC imebadilishwa jina na itakuwa ikiitwa FC Como.
Como FC yenye umri wa miaka 110 sasa ilishushwa daraja msimu uliopita kutoka Seria B mpaka Seria C baada ya kufilisika kiuchumi.Kwasasa Como FC inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Seria C na ina nafasi ya kurejea Seria B ikiwa itashinda michezo yake ya mtoano.
0 comments:
Post a Comment