Mshambuliaji wa Sports Club Villa aliesajiliwa huru msimu wa dirisha dogo, Emanuel Anold Okwi ameteuliwa kuwa nahodha wa kikosi cha timu ya timu ya Taifa ya Uganda "The Cranes"kitakachocheza mechi ya kirafiki machi 19 mwaka huu dhidi ya Eastern Region Select,mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Kamuli Town'
Okwi amejumuishwa kwenye hicho na kocha msaidizi wa The Cranes Moses Basena.
Boses Basena amefanya maamuzi hayo baada ya kuridhishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa ana goli sita kwenye ligi kuu nchini Uganda pia uzoefu wake na dhana ya uongozi katika timu kwa wenzake.
0 comments:
Post a Comment