728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 12, 2017

    Kumbe hata Conte anamgwaya Kante

    London,England.

    KAMA ilivyo desturi kuwa kila bosi ana bosi wake na kila mnyonge ana myonge wake basi kocha wa Chelsea,Antonio Conte ni mnyonge ile mbaya kwa kiungo wake wa shoka,Mfaransa N'Golo Kante.

    Unajua ishu iko vipi?Iko hivi Antonio Conte ameitazama safari yake ya soka ya miaka 19 ya kuvichezea vilabu vya Lecce na Juventus na kusema kuwa licha ya kwamba alikuwa jembe kali sana kwenye safu ya kiungo lakini Kante ndiyo habari ya mjini yaani jamaa ni mkali mpaka anaboa.

    Hata hivyo Conte amekataa kuwa mnyonge moja kwa moja mbele ya Kante kwa kadai kuwa kuna maeneo mengine alikuwa vizuri sana na Kante akasome. 


    Kante ni mchezaji imara (strong) sana kuliko nilivyokuwa mimi enzi zile nacheza soka.Lakini nafikiri nilikuwa bora kuliko yeye kwenye kupachika mabao tu lakini kwenye maeneo mengine jamaa kanifunika ile mbaya.Amesema Conte.

    Wakati huohuo Conte amesema kuwa yeye ni shabiki mkubwa sana wa wachezaji aina ya Kante ambao ni nadra sana kuwaona wakitembea uwanjani,muda wote wao ni kukimbia tu.Conte ameongeza kuwa ni muhimu kuwa na wachezaji kama Kante kikosini kama unataka kutwaa ubingwa.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kumbe hata Conte anamgwaya Kante Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top