Genk,Ubelgiji.
MTANZANIA Mbwana Samatta ameendelea kuwaonyesha wazungu kuwa hakwenda Ulaya kushangaa mataa hii ni baada ya leo mchana kuifungia Genk bao moja katika ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Westerlo katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Ubelgiji uliochezwa kwenye dimba ugenini la Het Kuipje.
Samatta aliiandikia Genk bao la kwanza katika dakika ya 7.Wakati Westerlo wakiwa bado hawaamini macho yao,Thomas Buffel aliifungia Genk bao la pili katika dakika ya 27 .Bao la tatu limetiwa kimiani na Omar Colley katika dakika ya 62 huku bao la nne likifungwa na Ruslan Malinovskiy katika dakika ya 90.
Aidha katika mchezo huo wenyeji Westerlo walilazimika kumaliza wakiwa pungufu baada ya Khaleem Hyland kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 65.
0 comments:
Post a Comment