728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, March 20, 2017

    Gareth Bale kufuata nyayo za Wayne Rooney

                                         Rangi nyeupe kichwani ni kipara kinachomwandama Bale

    Madrid,Hispania.

    STAA wa Real Madrid, Gareth Bale anafikiria kufuata nyayo za nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney kwa kufanyiwa upasuaji na kupandikizwa nywele kichwani ili kukwepa kipara kinachomwandama.

    Kwa mujibu wa gazeti la The Sun ni kwamba Bale amechoshwa na kipara hicho kilichopo katikati ya kichwa chake ambacho kwa muda mrefu amekuwa akikificha kwa kubana nyweli zake za kati kwa utepe wa kitambaa.

    Kwa mara ya kwanza kipara cha Bale kilionekana hadharani mwezi April mwaka jana kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Real Sociedad ambapo mvua kubwa ilinyesha na kufanya kipara kionekane.Mara ya pili ilikuwa ni kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 ulioisha kwa Wales kufungwa na Ureno.

    Kiungo wa Wales na Crystal Palace,Joe Ledley, 30,ambaye ni rafiki wa karibu wa Bale amedaiwa kupendekeza nywele za KSL ambazo hugharimu mpaka Paundi 10,000 kupandikizwa katika kliniki za Cardiff, Glasgow na Kent.Upandikizaji huchukua siku moja nzima kukamilika.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Gareth Bale kufuata nyayo za Wayne Rooney Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top