728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 11, 2017

    Dybala apiga moja,Juventus ikiibomoa AC Milan 2-1 Italia.


    Turin,Italia.

    Paulo Dybala (Pichani) akipiga mkwaju wa penati katika dakika ya 97 na kuipa Juventus ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AC Milan kwenye mchezo mkali wa Seria A uliochezwa Ijumaa usiku huko Juventus Arena.

    Mkwaju huo wa penati ulipatikana baada ya beki wa AC Milan,Mattia de Sciglio,kuunawa mpira wa krosi uliopigwa na beki wa kulia wa Juventus,Stephan Lichtsteiner.Kabla ya hapo AC Milan ilikuwa pungufu baada ya kiungo wake,Jose Sosa kutolewa uwanjani katika dakika ya 93 kwa kadi mbili za njano.




    Medhi Benatia ndiye aliyeanza kuifungia Juventus bao la kuongoza katika dakika ya 30 kabla ya Mshambuliaji wa Colombia,Carlos Bacca kuisawazishia AC Milan katika dakika ya 43.

    Ushindi huo umeifanya Juventus ijikite kileleni mwa msimamo wa ligi ya Seria A baada ya kufikisha pointi 70 pointi 11mbele ya Roma inayoshika nafasi ya pili na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa sita mfululizo wa taji la Scudetto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Dybala apiga moja,Juventus ikiibomoa AC Milan 2-1 Italia. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top