Dar es Salaam,Tanzania.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Mehbub Manji jana Ijumaa alitoa ufafanuzi kuhusiana na suala la mkataba wa klabu hiyo dhidi ya Kampuni ya Bia Tanzania.
Manji ameeleza ikiwa ni siku chache baada ya Yanga kuonekana wakiwa wamevaa jezi zenye nembo ya Quality Group badala ya Bia ya Kilimanjaro ambao wanajulikana ni wadhamini wao.
Yanga ilionekana kwa mara ya kwanza ikiwa imevaa jezi zenye nembo ya Quality Group wakati ikiivaa TP
Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho na kupoteza kwa bao 1-0
Katika taarifa yake, Manji ametoa ufafanuzi kuhusiana na mkataba huo.
MKATABA WA TBL NA YANGA
1.1.Mkataba wa kampuni ya bia nchini (TBL) na YANGA ulisainiwa miaka
mitano iliyopita na mtangulizi wangu.Huu ulikuwa mkataba haramu
kwani mamlaka ya kutia saini mikataba kwa mujibu wa Katiba ya Yanga yapo
kwa wadhamini na hapana kitu kama azimio kutoka bodi ya wadhamini kuingia katika makubaliano kama haya,au mkataba kusainiwa na wadhamini.
1.2.Wakati wa kipindi changu kilichopita, nilijitahidi kurekebisha tofauti zote zilizokuwepo, lakini nilishindwa. TBL ni mara moja tu imetoa mara moja tu Sh. 20 Millioni kwa ajili ya tamasha la Yanga Day zilizoahidiwa kutolewa kila mwaka, haijailipa klabu fedha ya marekebisho inayofikia Sh. 30 Milioni wala haijatupa basi kwa kiwango sahihi tulichotaka kama ililoahidi katika mkataba. TBL imejulishwa kuhusu hili lakini haijalishughulikia.
1.3.Yanga imeingia katika
mkataba wa masoko na kampuni ya International Marketing ili kupata
wafadhili wake, ili kupunguza pengo la
TBL kwa ajili ya mishahara ya Juni. Hii ni kampuni ambayo nilikuwa mwenyekiti wake na ikakubali ufadhili huo wa mwezi mmoja, jambo ambalo liliifanya Yanga
kuvaa jezi za nembo yake katika mchezo dhidi ya TP Mazembe.
1.4.Iwapo wanachama wa Yanga wakihisi nilivunja katiba kwa maslahi yangu binafsi au wakiwa na sehemu nyingine bora zaidi ya kufanya hivyo,walifikishe suala hilo kwenye kamati ya maadili ya klabu kwa ajili ya uamuzi.
YUSUF MEHBUB MANJI
MWENYEKITI KLABU YA YANGA
0 comments:
Post a Comment