728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 02, 2016

    MPASUKO:TAMBWE AJIAPIZA HATAKUJA KUMSAMEHE DONALD NGOMA KAMWE

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe,amesema kamwe hatoweza kumsamehe mchezaji mwenzake Donald Ngoma, kutokana na kile alichomfanyika nchini Uturuki kwa kumshambulia pasipo sababu za msingi.

    Tambwe amesema, amekutana na wachezaji wengi katika timu mbalimbali alizopitia ndani na nje ya nchi yake ya Burundi, lakini hakuwahi kugombana na mtu yeyote anashangazwa na kitendo kilichotokea kwa Ngoma.

    “Siwezi kumsamahe nilishamuahidi ingawa kocha na Nahodha walitukutanisha na kuyazungumza lakini ukweli imeniuma sana na sidhani kama naweza kumsamehe,”amesema Tambwe.

    Tambwe na Ngoma, walipigana wakiwa
    mazoezini nchini Uturuki jambo ambalo lilichafua hali ya hewa ya timu hiyo iliyokuwa ikijiandaa kuikabili TP Mazembe katika mchezo wa pili wa kombe la shirikisho Afrika.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPASUKO:TAMBWE AJIAPIZA HATAKUJA KUMSAMEHE DONALD NGOMA KAMWE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top