Liverpool, England.
Everton ikiwa chini ya Meneja Mpya Mholanzi,Ronald Koeman,imeanza kukiimarisha kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu England,hii ni baada ya kumsajili golikipa wa Uholanzi,Maarten Stekelenburg kutoka Fulham kwa ada ambayo imefanywa siri.
Stekelenburg,33,amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia timu hiyo ya Goodson Park baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya siku ya Ijumaa na jukumu lake kubwa la kwanza litakuwa ni kuvaa viatu vya aliyekuwa golikipa mkongwe za timu hiyo,Tim Howard aliyetimkia Colorado Rapids ya Marekani.
Hii ni mara ya tatu kwa Koeman kumsajili Stekelenburg.Mara ya kwanza ilikuwa katika timu ya Ajax na wawili hao wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa Uholanzi (Eredivisie) mwaka 2004.Mara ya pili ilikuwa ni Southampton alipomsajili kwa mkopo wa msimu mmoja.
Stekelenburg siyo mchezaji mdogo kwani mbali ya kucheza katika timu nyingi pia amejijengea sifa kubwa nyumbani kwao Uholanzi baada ya kuichezea timu yake ya taifa michezo 54 ikiwemo fainali ya kombe la dunia la mwaka 2010 iliyoishwa kwa Hispania kuifunga Uholanzi kwa bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment