Morogoro,Tanzania.
SIMON Msuva ameshindwa kuipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) baada ya mkwaju wake wa penati kuota mbawa katika mchezo ambao mabingwa hao watetezi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar kwenye dimba la Jamhuri,Morogoro jioni ya leo.
Mkwaju huo wa penati ulipatikana katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza baada ya mchezaji mmoja wa Mtibwa Sugar kunawa mpira akiwa ndani ya boksi na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo ilipaa juu ya lango la Mtibwa Sugar.
Hali ya mchezo
Timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini mashambulizi ya Yanga ndiyo yaliyoonekana kuwa makali zaidi huku Mtibwa Sugar wakionyesha uhai zaidi kwenye safu yao ya kiungo kuliko wapinzani wao.
Usalama.
Licha ya Uwanja wa Jamhuri leo hii kufurika mashabiki wenye itikadi tofauti lakini hali ya usalama ilikuwa shwari kabisa huku mpaka mwisho wa mchezo kukiwa hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani lililoripotiwa.
0 comments:
Post a Comment