728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 02, 2017

    Bao la Obrey Chirwa lilikuwa halali.

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    AFISA habari wa Ruvu Shooting ya Pwani,Masau Bwire,amesema bao la kichwa lililofungwa na mshambuliaji wa Yanga,Mzambia,Obrey Chirwa dhidi ya timu yake jana Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam lilikuwa halali.

    Bwire akiongea jana baada ya kuishuhudia timu yake ikichapwa mabao 2-0 na Yanga amesema anashindwa kujua kwanini mwamuzi,Ahmad Simba kutoka Kagera alikataa bao hilo wakati lilikuwa halali kabisa.

    Bwire ameongeza kuwa maamuzi ya mwanuzi Ahmad Simba katika mchezo huo pekee wa jana yaligubikwa na utata mwingi.Amedai matukio ya halali aliyafanya haramu na haramu aliyafanya halali ikiwemo kuipatia Yanga penati ambayo kwa muono wake anadai haikuwa halali.

    Wakati huohuo Bwire amesema kuwa Ruvu Shooting italiandikia barua ya malalamisho shirikisho la soka TFF kueleza machungu waliyonayo dhidi ya mwamuzi huyo alishindwa kutafsiri vizuri sheria 17 za soka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bao la Obrey Chirwa lilikuwa halali. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top