London,England.
Wa. kati dunia ikipambana kuondoa wimbi la matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni vilabu vya ligi kuu England vimekumbwa na kashfa ya kuwa na wachezaji wanaotumia dawa hizo zilizopigwa marufuku.
Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la The Sunday Times,Dr Mark Bonar wa Klinic ya Knightsbridge, London amedai kuwadunga sindano za kuongeza nguvu wanamichezo zaidi ya 150 wakiwemo wachezaji waliopo na waliowahi kucheza Arsenal, Chelsea,Leicester City na Birmingham City.
Bonar amesema kwa kipindi cha miaka sita iliyopita amekuwa akitoa huduma hiyo ya dawa ya Erythropoietin EPO na nyinginezo kwa wanamichezo wengi wa ndani na nje ya England wakiwemo waendesha baiskeli,wacheza tenesi,mabondia,wacheza kriketi na wanasoka.
0 comments:
Post a Comment