Manchester,England.
DALALI!!Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuitumia kuelezea kitendo alichokifanya kocha wa zamani wa Manchester United Alex Ferguson katika mchakato wa usajili wa Danny Welbeck kwenda Arsenal mwaka 2014.
Kwa mujibu wa mtandao wa Squwaka ni kwamba baada ya Louis van Gaal kumuweka sokoni Welbeck kwa madai kwamba hayuko katika mipango yake kwa vile tu hakuwa na makali kama ya Robin Van Persie ama Wayne Rooney,Ferguson alimpendekeza Welbeck kwa Arsene Wenger.
Ishu ilikuwa hivi!!Alex Ferguson aliyanyua simu akampigia Arsene Wenger na kumwambia msajili Welbeck,25 haraka.Van Gaal hamtaki.Ukishindwa kuitumia fursa hii adimu utakuwa mwendawazimu kaka!!.
Kisha Ferguson akaendelea kumpamba Welbeck kwa kumjaza sifa kedekede huku akimuita kuwa ni mchezaji msikivu sana na anayejua kufuata vyema maelekezo ya walimu wake.
Welbeck alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akitokea Manchester United kwa ada ya £16m siku ya mwisho kabisa ya usajili barani Ulaya.Mpaka sasa Welbeck amefanikiwa kuifungia Arsenal mabao 7 huku akiisaidia kutwaa kombe la FA msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment