Klabu iliyopanda daraja ya Watford imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji aliyechokwa katika klabu ya Liverpool Muitalia Mario Balotelli,25.
Sky Sports Italia imeripoti kuwa klabu hiyo iliyopanda ligi kuu msimu huu iko tayari kutoa kiasi cha £10m ambacho kinatakiwa na Liverpool ili kumruhusu nyota huyo mwenye vituko vingi kuhamia klabu nyingine.
Liverpool imemuweka Balotelli sokoni baada ya kutoridhishwa na kiwango chake tangu ajiunge nayo kwa ada ya £16m akitokea AC Milan ya nyumbani kwao Italia.
0 comments:
Post a Comment