Roma,Italia.
Unafiki kando!!Mlinda mlango wa Arsenal anayekipiga AS Roma kwa mkopo Wojciech Szczesny amesema anatamani kuona Leceister City ikitwaa ubingwa wa ligi kuu ya England msimu huu licha ya klabu yake ya Arsenal kuutaka pia.
Szczesny,24 akiongea na Sky Sport Italia amesema "Hakuna mtu yoyote katika mpira anayeweza kuielezea miujiza ya Leicester City akaeleweka.
"Japo mimi ni shabiki mkubwa wa Arsenal ligi kuu lakini natamani kuona kikosi cha Claudio Ranieri kikitwaa ubingwa msimu huu.Wamekuwa mfano na msukumo kwa kila mtu.Wanafurahisha kuwatazama jinsi wanavyocheza.
Wakati huohuo mlinda mlango huyo raia wa Poland ameweka wazi nia yake ya kubaki AS Roma moja kwa moja na kusisitiza kuwa tayari ameshaviambia vilabu vyote viwili juu ya mpango huo.
0 comments:
Post a Comment