Dar es salaam,Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Martin Chacha amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF kuanzia jana tarehe 5 Aprili 2016.
Katika barua yake aliyomwandikia Katibu
Mkuu wa TFF, Chacha alieleza kuwa amepata
majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho Martin alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Afisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria
nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
TFF inamtakia kila la kheri na mafanikio mema Chacha katika majukumu yake mapya.
0 comments:
Post a Comment