Lome,Togo.
Mfaransa Claude Le Roy leo ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Togo akichukua nafasi ya Tom Saintfiet aliyetimuliwa.
Le Roy,68 amesaini mkataba wa miaka mitatu na jukumu lake kubwa ni kuhakikisha Togo inafuzu michuano ijayo ya AFCON itakayopigwa mwakani nchini Gabon.
Togo wako nafasi ya tatu katika kundi lao wakiwa na pointi saba baada ya kushuka dimbani mara nne,pointi mbili nyuma ya vinara Liberia.Tunisia wako nafasi ya pili.
Kabla ya kutua Togo Le Roy amekuwa kocha Afrika kwa kipindi cha miaka thelathini. Baadhi ya mataifa aliyowahi kuyafundisha na kupata mafanikio ni Cameron, Senegal, DR Congo,Ghana na Congo Brazzaville.
0 comments:
Post a Comment