Manchester, England.
Bao la dakika ya 76 la winga Mbelgiji Kevin De Bruyne limeipeleka Manchester City katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada jumanne usiku kuilaza PSG kwa bao 1-0 katika mchezo wa pili wa robo fainali nyumbani Etihad.
Manchester City ambao katika mchezo wa kwanza waliibana PSG na kwenda nayo sare ya 2-2 huko Parc des Princes wangepata bao mapema lakini mshambuliaji wake Sergio Aguero alikosa penati kipindi cha kwanza iliyotolewa baada ya Muargentina huyo kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa PSG Kevin Trapp.
0 comments:
Post a Comment