728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 14, 2015

    FABIO CAPELLO ATUPIWA VIRAGO URUSI

    Kocha Fabio Capello hatimaye ametimuliwa kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya Urusi baada ya muendelezo wa matokeo mabovu.

    Capello ambaye alikuwa amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake amejikuta akipoteza kazi hiyo baada ya kushindwa kupata matokea mazuri katika michezo ya kutafuta nafasi ya michuano ya Ulaya (Euro 2016).

    Chini ya kocha huyo Muitaliano Urusi iliyo kundi G imeshinda michezo miwili,imefungwa miwili na kutoka sare mara mbili.Hivyo kwa matokeo hayo Urusi iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne pungufu kufikia mstari wa kufuzu.

    Wakati huo huo kocha wa CSKA Moscow Leonid Slutsky ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Urusi akichukua nafasi ya Fabio Capello.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FABIO CAPELLO ATUPIWA VIRAGO URUSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top