Roma,Italia.
Mshambuliaji mpya wa AS Roma Edin Dzeko raia wa Bosnia-Herzegovina ametamba kuipa mataji ya kutosha klabu hiyo kongwe ya Seria A.Dzeko aliyekamilisha usajili wake wa mkopo jana jumatano akitokea Manchester City kwa ada ya euro milioni 4 amesema ametua Roma kurudia kile alichokifanya England katika klabu ya Manchester City.Roma haijatwaa Seria A tangu mwaka 2000-2001.
Amesema [Nimekuja hapa kuisaidia Roma (Giallorossi) iweze kutwaa mataj,lakini yote haya yatafanikiwa tukiweka bidii uwanjani.]
Dzeko akiwa mazoezini AS Roma |
Akiongelea kilichomvutia zaidi Roma...Dzeko amesema [Ushawishi mkubwa umetoka kwa rafiki yangu Miralem Pjanic ambaye anacheza hapa .Mkurugenzi wa michezo Walter Sabbatini nae amefanya kazi kubwa.Wameniambia mengi mazuri kuhusu hapa hali ya hewa,mji na mshabiki.
![]() |
Jumla ya michezo aliyocheza Dzeko akiwa na Man City |
Dzeko ametua
Roma baada ya kuichezea Manchester City jumla ya michezo 185 na
kuifungia jumla ya magoli 71 huku mengi akiwa ameyafunga akitokea
benchi.Pia ametwaa mataji mawili ya ligi kuu,FA Cup mara moja,Ngao ya
jamii mara moja na Capital One Cup mara moja.Roma itamsajili jumla Dzeko msimu ujao kwa ada ya euro milioni 11.
![]() |
Dzeko akisaini mkataba |
0 comments:
Post a Comment