728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 13, 2015

    MMALI WA SIMBA SC HATARI TUPU


    STRAIKA anayekuja kufanya majaribio Simba raia wa Mali, Makan Dembele, anatua Msimbazi akiwa na rekodi ya kuridhisha katika ufungaji mabao, lakini pia akiwa na ‘kismati’ cha kucheza mechi za kwanza bila kupoteza.

    Dembele aliyezaliwa Desemba 25, 1986 kwa sasa akiwa na umri wa miaka 29, ni mchezaji mwenye mwili uliojengeka vilivyo kumwezesha kupambana na mabeki wakorofi wa aina ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga na Agrey Morris wa Azam.

    Juu ya suala zima la ufungaji mabao katika timu zote alizowahi kuchezea, amekuwa na wastani wa kufunga mabao 0.7 kwa kila mechi, ukiwa ni mzuri wenye kumfanya kuwa mmoja wa wafungaji tishio.

    Akiwa na klabu ya USFAS Bamako ya Mali msimu wa 2005-2006, alifunga mabao kumi na moja ndani ya mechi 20, Gostaresh Foolad (2006-2007) mabao 16 mechi 23, Raja De Casablanca (2007-2008) mabao nane mechi 14 na alipokuwa katika klabu ya Aboomoslem msimu wa 2008-2009, alifunga mabao 18 ndani ya 26.


    Msimu wa 2009-2012 akiwa na klabu ya Shahrdari Bandar Abbas, alicheza mechi31 na kufunga mambao 21, wakati baada yak utua JS Kabylie ya Algeria, msimu wa 2012-2013 alicheza mechi 16 na kucheka na nyavu mara tisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MMALI WA SIMBA SC HATARI TUPU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top