Lameck Francis
Pemba,Zanzibar.
Timu ya Shaba ya kisiwani Pemba imesema haina mpango wa kwenda uwanjani kucheza tena na Chipukizi katika mchezo uliopangwa kuchezwa kwa dakika 4 tu hapo kesho Jumatano baada ya mchezo wa awali uliochezwa Ijumaa iliyopita kudaiwa kuvunjwa kabla ya dakika 90
Akizungumza na soka extra Kocha Msaidizi wa Shaba Shaame Hamad amesema Shaba haijaelezwa sababu zitokanazo na kanuni juu ya kurejewa mchezo huo kwa dakika nne ili wakubaliane na matakwa ya chama cha mpira kisiwani zanzibar (ZFA) inatakiwa iwape sababu za msingi za kurejewa kwa mchezo huo.
Aidha kocha huyo amesema pamoja na kuelezwa sababu ni lazima ZFA iwagharamie kwenda uwanjani kwa ajili ya mchezo huo, huku wakitaka mchezo uchezwe nje ya uwanja wa Gombani ambao ndio ulitumika kwa mechi ya kwanza wakidai hawawezi kucheza na timu hiyo moja kwenye uwanja mmoja tu kwa vile kuna taratibu za kucheza nyumbani na ugenini.
timu ya shaba ndio timu yenye mashabiki wengi na inanguvu kubwa kisiwani pemba,pamoja na hayo yote pia timu hiyo inasifa ya kufanya vurugu sana ndani ya uwanja na nje ya uwanja ambapo mashabiki wake huanzisha pale wanapoona mwamuzi hazitendei haki sheria 17 za mpira.
kwa upande wao Chipukizi kupitia kwa katibu wake Adam Abdalla wamesema licha ya kusikitishwa na uamuzi huo wa ZFA kurejewa kwa mchezo huo badala ya chama hicho kutumia kanuni kuwapa ushindi wao wakidai Shaba ndio walioanzisha vurugu hizo.
Ligi kuu ya Zanzibar mpaka kufikia hivi sasa inachezwa kwa kanda mbili tofauti ambazo ni Unguja na Pemba ambako kila kanda ina timu 18 hivyo jumla kuwa 36.
0 comments:
Post a Comment