Dar Es Salaam,Tanzania.
KOCHA wa Yanga SC,Mzambia George Lwandamina "Chicken" kwa mara ya kwanza amemuweka benchi kinara wa mabao wa klabu hiyo,Simon Msuva katika kikosi kitakachoivaa Kiluvya FC kwenye mchezo wa kiporo wa kombe la Azam Confedaration Cup jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa,jijini Dar Es Salaam.
Wakati Msuva akianzia benchi chipukizi Yusufu Mhilu ndiye aliyepewa jukumu la kucheza kama winga wa kulia siku ya leo.
Kikosi Kamili
1. Deogratius Munishi
2. Hassan Kessy
3. Oscar Joshua
4. Vicente Bossou
5. Nadir Haroub
6. Juma Saidi
7. Yusufu Mhilu
8. Deusi Kaseke
9. Obrey Chirwa
10. Juma Mahadhi
11. Geofrey Mwashuiya
Akiba
- Ali Mustafa
- Andrew Vicent
- Kelvin Yondani
- Saimoni Msuva
- Justine Zulu
- Malimi Busungu
- Emanuel Martin
Mshindi kati ya timu hizo, itaungana na timu nyingine saba zilizotangulia kucheza Robo Fainali ambazo ni Simba na Azam FC za Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha, Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni. Bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment