728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 07, 2017

    Ligi ya mabingwa Ulaya:Je,Arsenal kupindua matokeo leo dhidi ya Bayern Munich?


    London,England.

    Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya timu 16 ya UEFA CHAMPIONI LIGI, zinaanza 
     kuchezwa leo Jumanne Machi 7 kwa Mechi 2.
    Huko Emirates Jijini London, Wenyeji Arsenal wanapaswa kupindua kipigo cha 5-1 walichoshushiwa na Bayern Munich katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Ujerumani.
    Ili kufuzu kuingia Robo Fainali, Arsenal wanapaswa kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika kwa kushinda 4-0 au kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 4-0.
    Mesut Ozil is back after a bout of illness

    Mechi ya Pili ya leo ni huko Naples, Italy wakati Napoli ikirudiana na Mabingwa Watetezi ,Real Madrid huku wakihitaji ushindi wa bao 2-0 kwa kuwa mchezo wa awali walichapwa 3-1 huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Spain kwenye Mechi ya Kwanza.
    Napoli pia wanaweza kufuzu ikiwa watashinda kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 2-0.
    Kesho ,Jumatano Machi 8 zipo Mechi nyingine 2 ; Barcelona na Paris Saint Germain,huku PSG wakiwa mbele 4-0 na mechi ya pili ni kati ya Borussia Dortmund na Benfica huku Benfica wakiongoza 1-0.
    Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitakamilika Wiki ijayo, Machi 14 na 15, kwa Mechi nyingine 4 ili kutoa Washindi watakaocheza Robo Fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi ya mabingwa Ulaya:Je,Arsenal kupindua matokeo leo dhidi ya Bayern Munich? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top