Dar Es Salaam,Tanzania.
MABAO manne ya Mzambia,Obrey Chirwa,yameipeleka Yanga robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho (Azam Sports Confederation Cup) katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Kiluvya United kwenye mchezo wa kiporo wa hatua ya sita uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru,Dar Es Salaam.
Geoffrey Mwashiuya alianza kuifungia Yanga bao la kwanza katika dakika ya 11 kwa mkwaju mkali baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mtogo,Vincent Bossou.
Obrey Chirwa aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 22 akiunganisha krosi safi ya Juma Mahadhi kutoka wingi ya kulia kisha akaongeza mabao mengine katika dakika za 48,70 na 88.
Bao jingine la Yanga limefungwa na Juma Mahadhi katika dakika ya 74 huku lile la kufutia machozi kwa upande wa Kiluvya United,likifungwa na Edgar Mfukamule katika dakika 40.
Kwa ushindi huo sasa Yanga itakutana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa robo fainali.
0 comments:
Post a Comment