728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 10, 2017

    Victor Wanyama akataa kuwa mwanasiasa

    NAIROBI, Kenya.

    KIUNGO mkabaji wa Kenya na Tottenham Hotspur, Victor Wanyama amesema kuwa hafikirii hata kidogo kuja kuwa mwanasiasa pindi atakapokuwa amestaafu kucheza soka.

    Wanyama ama ‘Big Vic’ kama anavyoitwa na wachezaji wenzake wa Tottenham Hotspur ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mtangazaji maarufu wa michezo ya ligi kuu England,John Dykes.

    Wanyama mwenye umri wa miaka 25 sasa amemwambia Dykes kuwa lengo lake kuu si kuwa mwanasiasa kama wafanyavyo nyota wengi wa Afrika pindi wanapostaafu soka.

    Lengo lake ni kufungua shule ya soka (Football Academy) nyumbani kwao Kenya kwa ajili ya kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wadogo ili waweze kutimiza ndoto za kucheza ligi kubwa za Ulaya kama ilivyo kwake.



    "Nisingependa kuwa mwanasiasa.Nitapenda kuisaidia Jamii yangu ya Kenya kuwa na vifaa ( facilities) bora vya soka kama tulivyonavyo hapa England.Vifaa ambavyo vitabadili sura ya soka letu kwa kuwapatia watoto elimu stahiki ya soka ili pindi watakapojiunga na vilabu vya Ulaya wawe tayari wamekwisha wiva.

    Tayari Wanyama ameshaanza taratibu kutimiza ndoto za watoto wengi wa Kenya kwa kufanya nao mazoezi pindi anapokuwa mapumzikoni pamoja na kuwapa msaada wa jezi ambazo amekuwa akizichukua kutoka England.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Victor Wanyama akataa kuwa mwanasiasa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top