728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 02, 2017

    Ukweli kuhusu kuuzwa kwa klabu ya African Lyon

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    BAADA ya jana Jumatano kuibuka habari kuwa klabu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) kuwa mbioni kuuzwa kwa kampuni ya GSM Limited ya jijini Dar Es Salaam,leo mmiliki wa klabu hiyo, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ ameibuka na kusema kuwa habari hizo si za kweli na ni uzushi mtupu.

    Akifanya mahojiano na kituo cha redio cha EFM kupitia kipindi chake cha michezo cha asubuhi cha Sports HQ,Zamunda amekana kuwa kwenye mazungumzo ya kuiuza klabu hiyo inayoshika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu.

    Kwa msisitizo na masikikito makubwa,Zamunda amesema hana mpango wa kuiuza African Lyon leo wala kesho na kusisitiza kuwa hajawahi kukaa meza moja na kampuni ya GSM kujadili mpango wa kuiuza klabu hiyo.Ikumbukwe kampuni ya GSM ndiyo wadhamini wa klabu ya Majimaji FC ya Songea.

    Zamunda alianza kuimiliki African Lyon mwaka 2010 baada ya kuinunua kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wake wa awali Mohammed Dewji maarufu kama Mo".

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ukweli kuhusu kuuzwa kwa klabu ya African Lyon Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top