Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL),inatarajiwa kuendelea tena leo Jumamosi kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja vinne tofauti.
Vinara wa ligi hiyo Simba watakuwa wenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kagera Sugar itaikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Michezo mingine inayotarajiwa kuvurumishwa leo ni kati ya Toto Africans na Mbao FC utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.Azam FC itakuwa nyumbani Chamazi Complex kupepetana na Stand United ya Shinyanga.Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni wakati michezo mingine itaanza saa 10.00 jioni.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumapili Machi 5,2017 kwa michezo miwili kuchezwa ambapo Wakata Miwa,Mtibwa Sugar watakuwa Jamhuri Morogoro kuwakabiri mabingwa watetezi Young Africans.African Lyon watakuwa Uwanja wa Uhuru kuwaalika Mwadui kutoka Shinyanga.
Jumatatu Machi 6, mwaka huu. Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
0 comments:
Post a Comment