728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 08, 2017

    Zanzibar yaanzisha mchezo mpya wa Taikondo


    Lameck Francis
    Unguja,Zanzibar.

    Zanzibar imeanzisha mchezo mpya wa taikondo ambapo asili yake ni kutoka Korea na kuenea katika nchi nyingine Kocha mkuu wa mchezo huo Maximilian Kaingala kutoka Tanzania bara kwa sasa yupo kisiwani unguja kusambaza mchezo huo.

    Akizungumza na soka extra kocha maxmilian amesema mafunzo hayo ni ya awali ,na hufanyika kila baada ya miezi 3 ili huwasaidia wachezaji wa mchezo huo kuwa na uvumilivu na kutokata tamaa katika maisha . 
    tumezungumza na mmoja wa wachezaji wa mchezo huo Saada Khathani  kutoka Tanzania Bara amesema kwaupande wake ameupenda mchezo huo,kwakua  ni mchezo ambao unaweza kukusaidia, heshima na uvumilivu, sehemu yoyote huku akiwataka Wanawake wa Zanzibar kujitokeza kujiunga katika mchezo huo kwani unafaida sana.

    Pia toka umetambulishwa mchezo wa taikondo kumejitokeza kwa vijana wadogo kabisa na Kijana mdogo kuliko wote Sabri Ali ambaye ameshiriki  mchezo huo,amezungumza namna alivyoupokea kuwa anaimani utamletea manufaa pamoja na kushukuru familia yake kwa kumruhusu kujifunza mchezo huo.

    Mchezo huo unafundishwa katika ukumbi wa Judo Amani kwa kila siku zaJumatatu, Jumatano na Alhamis kuanzia saa 1:00 usiku hadi 3:00 usiku, nakuombwa watu kujitokeza ili kujifunza mchezo huo pamoja na wadau ambao wanaweza kusapoti ili kufika malengo yake.

    Sehemu ya viambatisho
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Zanzibar yaanzisha mchezo mpya wa Taikondo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top