Accra,Ghana.
HATA IWEJE staa wa Ghana,Sulley Muntari,hawezi kuoa mke wa pili licha ya imani yake kumruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja.Hii ni kwa mujibu wa mke wake,Menaye Donkor.
Donkor,35,Miss Universe Ghana 2005 amesema kuwa kabla ya kufunga ndoa walifikia makubaliano na Muntari alimuhakikishia kuwa hataoa mke mwingine na yeye [Donkor] ndiye atakayekuwa mke wake wa pekee.
"Sulley daima yuko nyumbani na ninajua kile nilichonacho nyumbani.Kamwe hajawahi kuniambia kuwa anataka kuoa mke wa pili licha ya kwamba yeye ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu.
Tulipokutana kwa mara ya kwanza,tulikaa chini na kuzungumzia hilo na akaniambia kuwa baba yake alioa mke mmoja pekee hivyo na yeye angependa mimi ndiye niwe mke wake wa pekee.
0 comments:
Post a Comment