Turin,Italia.
KOCHA wa Juventus, Massimiliano Allegri,amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba atajiunga na Arsenal katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya. Hii ni kwa mujibu wa gazeti la michezo la Italia,CalcioMercacto.
Allegri,49,kocha wa zamani wa AC Milan, Cagliari na Sassuolo,katika siku za hivi karibuni amekuwa akitajwa kwenda kuchukua nafasi ya Arsene Wenger,67,Ambaye amebakiza miezi minne kufikia mwishoni mwa mkataba wake huku kukiwa hakuna taarifa rasmi kama atasaini mkataba mpya ama la.
Imedaiwa kuwa Allegri akiwa katika maongezi huku akipata mlo wa mchana kwa bahati mbaya aliwadokeza marafiki zake kuwa atajiunga na Arsenal iliyoko kaskazini mwa jiji la London.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tu tangu Allegri agombane na nyota wake wawili wa kutumainiwa mshambuliaji klabuni Juventus,Paolo Dybala na beki Leonardo Bonucci.
Huku ugomvi wake na Bonucci ndiyo ukidaiwa kumuumiza zaidi hasa baada ya uongozi wa Juventus kushindwa kumpa sapoti ya kutosha katika kumwajibisha beki huyo wa Italia.
Wakati huohuo taarifa kutoka jijini Turin zinasema tayari Juventus imeshaanza mikakati ya kumpata mrithi wa Allegri na kuna habari kuwa imevutiwa na kocha wa AS Roma,Luciano Spalletti.
0 comments:
Post a Comment