Simba Nhivi
Singida,Tanzania.
TIMU ya Singida United ambayo imerejea kwa mara nyingine kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya kupotea kwa miaka mingi imeripotiwa kuwa mbioni kukiongezea nguvu kikosi chake tayari kwa msimu mpya wa ligi hiyo kwa kuwasajili nyota watatu wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe.
Nyota wanaodaiwa kukaribia kabisa kumwaga wino kwenye karatasi nyeupe ni mabeki Elisha Muroiwa wa Dynamos na Simba Nhivi wa CAPS United pamoja na kiungo mshambuliaji wa Chicken Inn,Raphael Kitinyu.
“Nakwenda kusaini mkataba mpya.Siendi kufanya majaribio bali nakwenda kumalizia mazungumzo na kusaini mkataba.Nafahamu Singida United watanisajili muda si mrefu.Amesema Kitinyu ambaye mkataba wake na Chicken Inn unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Ikiwa sajili hizo zitakamilika ligi kuu bara msimu ujao itakuwa na jumla ya nyota saba kutoka Zimbabwe Bruce Kangwa (Azam FC),Method Mwanjali (Simba SC),Donald Ngoma na Thabani Kamusoko (Yanga).
0 comments:
Post a Comment