Genk,Ubelgiji.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Samatta (Pichani) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia KRC Genk mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 ya vinara wa sasa wa ligi kuu Ubelgiji,Club Brugge huko Luminus Arena,Genk.
Samatta amefunga mabao hayo katika dakika za 5 na 42 akitumia vyema pasi maridhawa kutoka kwa viungo Malinovsky na Alejandro Pozuel.Bao la Club Brugge limefungwa na José Izquierdo katika dakika ya 43.
Ushindi huo umeifanya KRC Genk ifikishe pointi 45 na kushika nafasi ya 8 baada ya kushuka dimbani mara 29.Licha ya kichapo Club Brugge bado wako kileleni na pointi zao 58.
0 comments:
Post a Comment