London,England.
WACHEZAJI wa Bayern Munich (Pichani) wakimpongeza Robert Lewandowski baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 55 katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Arsenal dimbani Emirates kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Mabao mengine ya Bayern Munich yamefungwa na Arturo Vidal aliyefunga
mabao mawili dakika za 50
na 85.Arjen Robben dakika ya 68 na Douglas Costa dakika ya 78.Bao pekee la Arsenal limefungwa na Theo Walcott katika dakika ya 20 huku nahodha wake Laurent Koscielny akitolewa kwa kadi
nyekundu dakika ya
54.
Ikumbukwe katikamchezo wa awali Bayern Munich iliichapa Arsenal kwa mabao 5-1hivyo imetinga robo final I kwa jumla ya ushindi wa mabao 10-2.
Wakati huohuo mashabiki wenye hasira wa Arsenal muda mfupi baada ya kichapo hicho kizito wameonekana wakiwa na mabango ya kuutaka uongozi wa klabu hiyo kutomwongeza mkataba mpya kocha, Arsene Wenger pindi ule wa sasa utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu.
Mashabiki hao wanaona muda wa Wenger kuondoka na kuiacha klabu yao umefika.Aondoke ili kupisha watu wengine watakaokuja na changamoto mpya.
0 comments:
Post a Comment