Barcelona,Hispania.
IKICHEZA nyumbani Camp Nou,Barcelona imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi ya La Liga baada ya Jumatano usiku kuitandika Sporting Gijon kwa mabao 6-1.
Lionel Messi alianza kuipa Barcelona uongozi baada ya kuifungia bao la kwanza katika dakika ya 9 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo Javier Mascherano.
Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Juan Rodriguez, aliyejifunga,Luis Suarez,Paco Alcacer,Ivan Rakitic na Neymar Jr.Bao pekee la Sporting Gijon limefungwa na Carlos Castro.
Ushindi huo umeifanya Barcelona ifikishe ponti 57 na kukaa kileleni baada ya kucheza michezo 25.Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya pili wakiwa na pointi 56 katika michezo yao 24 hii ni baada ya Jumatano usiku kulazimishwa sare ya 3-3 na Las Palmas.
Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga mara. mbili na Isco Alcarcon huku Gareth Bale akilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.Las Palmas wao walijipatia mabao yao kupitia kwa Jonathan Viera aliyefungwa kwa mkwaju wa penati,Tana na Mghana Kevin-Prince Boateng.
0 comments:
Post a Comment